
Muundo wa shairi hujikita katika mpangilio wa mishororo, beti, vina, na kibwagizo. Washairi hutumia mitindo tofauti ili kuwasilisha ujumbe wao kwa njia ya kipekee. Aina mbalimbali za mashairi kulingana na muundo wake ni kama ifuatavyo:
- Sabilia - Shairi lisilo na kibwagizo. Kituo cha mwisho katika kila ubeti hubadilika, hivyo kila ubeti huwa na kiishio kinachojitegemea.
- Kikwamba - Shairi ambalo neno moja au kifungu cha maneno hurudiwarudiwa mwanzoni mwa mishororo au beti ili kusisitiza ujumbe.
- Pindu ni aina ya shairi ambapo neno la mwisho la mshororo wa mwisho wa ubeti hutumika kama mwanzo wa mshororo wa ubeti unaofuata.
Uainishaji wa mashairi kwa kuzingatia muundo huangazia mtindo wa upangaji wa mishororo, beti, vina, na kibwagizo. Mashairi kama Sabilia, Sakarani, Kikwamba, na Pindu huonyesha ubunifu wa washairi katika kutumia vipengele vya lugha ili kufanikisha lengo lao la kisanaa na kifasihi.
102
2
Maoni ya Wasomaji
Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.
Andika Maoni
Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.