Ataitwa Mnazarayo
Ameposiwa Mariamu, na Yusufu mwenye haki,
Nalo jambo la muhimu, jambo Yusufu hataki,
Ana mimba Mariamu, Yusufu atahamaki,
Haya yote twayasoma, nyarakani takatifu.Ni malaika kwa ndoto, anamwambia Yusufu,
Atampata mtoto, Mariamu asihofu,
Si ajabu hilo pato, ni Roho Mtakatifu,
Usihofu kwa lolote, haya yote yalinenwa.Yeye atazaa mwana, jinale Imanueli,
Yeye ni Mungu maana, Pamoja nasi kwa kweli,
Huyo mwana mwenye jina, aokoe bila swali,
Yusufu umsharifu, huyo mwana ni mfalme.Mamajusi wamkafika, toka kwao mashariki,
Kumuona wakitaka, huyo mwenye kibariki,
Herode kafadhaika, hilo jambo halitaki,
Ataka yeye pekee, ukuu aumiliki.Bwana wapi azaliwa, Herode akauliza,
Papo hapo kajibiwa, kishaye wakimweleza,
Bethilehemu azawa,ufalme tapoteza,
Nayo hii ni taarifa, ikampa hangaiko.Mwokozi amezaliwa, himaya yote ni yake,
Atakayebarikiwa, na Maulana babake,
Heri atakayekuwa, akiyaamini yake,
Hakikisha ndani yako, mwokozi amezaliwa.Herode akawatuma, wale mamajusi wote,
Akawaamuru hima kutafuta Kristo kote,
Herode kwa taadhima, kumshujudu apate,
Uzuri wa mkakasi, ndani kipande cha mti.Wakaongozwa na nyota, hadi alikozaliwa,
Kristo dhahabu kapata, uvumba pia akawa,
Manemane,kwa kitita, zile zote akapewa,
Hizi zote ni zawadi,alipewa mfalme.Mungu naye kawajia, Mamajusi kama ndoto,
Mungu akawaambia, yeye hataki mtoto,
Wasiende yake njia, ataka afe mtoto,
Wale wote mamajusi, wakapitia nyingine.Yusufu kawachukua, Mwokozi na mama yake,
Baada ya kutambua, kutoka kwa mola wake,
Herode ataamua, hataki Mwokozi kwake,
Wakaelekea Misiri, na kukaa kule wote.Herode lipofariki, wakaandamana wote,
Mwana-Herode kabaki, himaya naye apate,
Naye mwenye kubariki, Nazareti akupate,
Manabii walinena, taitwa Mnazarayo.
Shairi hili linaeleza simulizi la kuzaliwa kwa Yesu Kristo, kama linavyopatikana katika Maandiko Matakatifu. Linafuatilia matukio kutoka kwa Mariamu kupokea mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu, hadi familia ya Yesu kuhamia Nazareti baada ya hatari kutoka kwa Mfalme Herode.
Shairi linaeleza kwa kina jinsi mpango wa kimungu ulivyotekelezwa kwa njia ya ajabu na ya kiroho, na jinsi watu wa kawaida kama Mariamu na Yusufu walivyotumika katika historia ya wokovu. Pia linaonyesha kuwa Yesu alizaliwa si kwa kawaida, bali kwa kusudi la kuleta wokovu kwa wanadamu.
Lengo kuu
Lengo ni kufundisha hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo, kuonyesha ukuu wa mpango wa Mungu kwa watu, na pia kuhimiza imani, unyenyekevu, na utiifu kwa maongozi ya kiroho. Pia linaweka bayana hatari zilizokuwapo na ulinzi wa Mungu dhidi ya njama za Herode.
Mandhari
Mandhari ya shairi ni ya kiroho na kihistoria, ikianzia Bethlehemu hadi Misri na kurudi Nazareti. Linaelezea mazingira ya maisha, wasafiri kutoka mashariki, hofu ya watawala, na uongozi wa kimungu kupitia ndoto na ishara.
Hadhira Inayolengwa
Shairi linaelekezwa kwa watu wa imani ya Kikristo, wanaopenda kujifunza kwa njia ya ushairi kuhusu hadithi ya kuzaliwa kwa Kristo. Linafaa pia kwa watoto, waumini, na matukio ya Krismasi kwa namna ya fasihi simulizi.
Msimamo wa Mtunzi
Mtunzi ana msimamo wa kiimani na kiroho, akiwasilisha hadithi ya Biblia kwa njia ya heshima, utulivu na uzito wa maana. Anasisitiza kuwa Yesu ni mfalme aliyezaliwa kwa kusudi kubwa, na kwamba watu wote wanaalikwa kumwamini na kumpokea.
Maoni ya Wasomaji
Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.
Andika Maoni
Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.
Ingia kwa Google ili kutoa maoni kwa jina lako.