Shairi Guni Katika Ushairi wa Kiswahili

Tarehe: Machi 21, 2025 - Kimani wa Mbogo

Shairi Guni ni utungo wa kishairi unaoonekana kwa sura kuwa shairi, lakini hauzingatii kikamilifu kanuni za arudhi. Hilo linaweza kuwa kwa kutofuata mizani, vina, au mpangilio wa vipande katika mishororo. Ingawa lina ladha ya kishairi, shairi-guni linakosa usahihi wa kitaalamu katika ujenzi wa mashairi ya kimapokeo.

Mwandishi anaweza kutunga shairi lenye dhamira nzuri na lugha ya kishairi, lakini likakosa urari wa sauti, idadi sawa ya silabi, au vina vinavyolingana, hivyo kuwa shairi-guni.

Mfano wa Shairi Guni

Nilikupenda kwa moyo
Nikakuamini bila mashaka
Lakini sasa ni tofauti
Umekuwa mtu mwingine

Ufafanuzi

  • Muundo, ni shairi: lina mishororo minne na lina dhamira ya mapenzi yaliyovunjika
  • Lakini:
    • Hakuna mizani ya silabi inayolingana (mistari ina idadi tofauti ya silabi)
    • Vina vya mwisho havafuatani wala kufanana
    • Hakuna mpangilio wa vina wa kimapokeo
    • Hakuna matumizi ya vipande kama ukwapi na utao

Hivyo, licha ya kuwa na hisia, dhamira na mpangilio wa mistari, utungo huu ni shairi-guni, si shairi halisi la kimapokeo.

91 1

Maoni ya Wasomaji

Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.

Andika Maoni

Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.