
Vipande katika mashairi vinarejelea sehemu zinazojitokeza ndani ya mshororo mmoja. Mashairi yanaweza kuwa na vipande viwili, vitatu, au hata vinne katika kila mshororo. Vipande hivi vinaweza kufuata vina maalum au kubadilika kwa mpangilio tofauti. Hapa tunajadili baadhi ya aina kuu za mashairi kulingana na vipande vyake.
- Mathnawi - Shairi ambalo kila mshororo una vipande viwili. Mashairi mengi ya Kiswahili yametungwa kwa kutumia mtindo huu. Vipande viwili vya mshororo hutenganishwa kwa alama ya ‘koma’, na kila kipande kina vina vyake.
- Ukawafi - Shairi ambalo kila mshororo una vipande vitatu, vinavyojulikana kama:
- Bantudi - Shairi ambalo kila mshororo una vipande vinne, na kila kipande kina vina vyake. Hii ina maana kuwa mshororo mmoja unakuwa na vina vinne vinavyofanana.
Uainishaji wa mashairi kwa kuzingatia vipande huonyesha jinsi mshairi anavyogawanya mshororo wake ili kuleta mpangilio wa vina na mdundo wa kishairi. Aina kama Mathnawi, Ukawafi, na Bantudi zinaonyesha upekee wa mashairi ya Kiswahili katika mpangilio wa vipande ndani ya mishororo.
Maoni ya Wasomaji
Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.
Andika Maoni
Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.