
Mashairi ya Kiswahili huweza kuainishwa kulingana na dhamira yake, yaani lengo kuu au maudhui yanayozingatiwa katika utunzi. Dhamira hizi huathiri mtindo, matumizi ya lugha, na ujumbe wa shairi. Zifuatazo ni aina za mashairi zinazotokana na uainishaji huu.
- Zivindo - Mkondo wa mashairi unaojengwa kwa maana mbalimbali za maneno kutolewa kupitia mafumbo.
- Malumbano - Mashairi haya huweza kuwa ya majibizano, mabishano, au mashindano ya lugha ambapo washairi hujaribu kushinda wenzao kwa hoja, ustadi wa lugha, au ubunifu wa vina na mizani.
- Taabili - Mashairi yanayotungwa kwa nia ya kumsifia au kumkumbuka mtu aliyefariki.
Uainishaji wa mashairi kwa kuzingatia dhamira huonyesha namna mashairi yanavyobeba ujumbe wa kina, iwe kwa kujifunza, kubishana, au kuomboleza. Ushairi huu huendeleza lugha, kuburudisha, na kutoa mafunzo kwa jamii kupitia mbinu mbalimbali za kifasihi.
114
5
Maoni ya Wasomaji
Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.
Andika Maoni
Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.