Ukingoni Tumefika 
Ukaraguni • Urafiki

Ukingoni Tumefika 

Tarehe: Oktoba 1, 2003 - Kimani wa Mbogo

Ukingoni Tumefika 

Siku yangu imefika, nisemayo kwaherini,
Nawapeni kwa hakika, mkono wa buriani,
Nawatakia baraka, na fanaka maishani,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Kuwa hapa sakafuni, miaka nne si haba,
Kiongozi ni mbioni, mekuwa bila msiba,
Shukrani nawapeni, kwa kufuata ratiba,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Bwana kwetu awe njia, ukweli pia uzima,
Nawe usije kulia, nayo dumia kuhama,
Salama na wewe pia, nakuombea Karima,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Wavyele wangu wasema, niwasalimie nyote,
Kila siku wanituma, huko kwenu enyi nyote,
Fanya bidii kwa hima, mbio zenu mzipite,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Banati tangu kuhama, mbioni nimekujuwa,
Nayo mambo mengi hima, kinaganaga kujuwa,
Mengine yakiwa rima, karibu kuniunguwa,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Muhula wa kwanza wewe, wanishinda Kiswahili,
Halafu nacho kiwewe, chakufuata wa pili,
Sheng'i italiki wewe, kifuate kiswahili,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Uyajuavyo kinaga uyaache sakafuni,
Nayo moyo kuupiga, yasiweze maishani,
Sikio nalo kutega, yote haya maanani,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Mbioni ukihitimu, tie nanga sakafuni,
Ujichunge na ghulamu, kero siwe maishani,
Wasije kukuhujumu, uoze bila idhini,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Wewe tumekuwa nawe si kidogo dawatini,
Sasa utengano uwe, tumeshatoka mbioni,
Wewe siti bora uwe, mwenye hekima bongoni,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Lipate hili muhimu, ulitie maanani,
Mimi nilikufahamu, we zamani imanini,
Sasa una roho ngumu, ukapoteza imani,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Hata ukiwa polisi, ama ukiwa yeyote,
Pia uwe mtu mwasi, na ujulikane kote,
Nawe bila Mola basi, yatakuwa bure yote,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Sitasahau sikiza, uyatie ubongoni,
Nayo sio ya kutweza, huwa ada maishani,
Ili usije punguza, wala kuongeza sini,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

Famasisti ukiwa, yakini pia msusi,
Mdubira weza kuwa, na ahera uihisi,
Ghulamu wazo ondowa, na usiwe na utesi,
Ukingoni tumefika, mbio zifike hatima.

© Kimani wa Mbogo

Shairi hili ni la kuaga baada ya kuhitimu kidato cha nne, likielezea safari ya elimu iliyofikia ukingoni. Mtunzi anatumia lugha ya heshima na shukrani kuwaaga wenzake, walimu, na shule, huku akitoa nasaha na matumaini kwa siku zijazo.

Shairi lina ujumbe wa kuhitimu kwa mafanikio na kuagana kwa heshima na upendo. Mtunzi anawakumbusha wenzake kuhusu safari yao ya pamoja shuleni na changamoto walizokumbana nazo, lakini zaidi anasisitiza kuwa mwisho huu si wa huzuni, bali wa furaha na matumaini. Anawaombea baraka na mafanikio katika maisha ya baadaye, huku akiwasihi wadumishe maadili, heshima, na bidii. Pia kuna ujumbe wa kiroho—kumuomba Mungu awe mwongozi wao katika njia ya maisha.

Lengo kuu

Lengo kuu la mtunzi ni kutoa shukrani kwa waliomsaidia katika safari ya elimu, kuaga wenzake kwa staha, na kuwaasa kuhusu maisha ya baadaye. Anatumia shairi hili kama njia ya kuacha alama ya ukumbusho na kuonyesha kwamba amekomaa kifikra na kiroho. Aidha, anawapa motisha wenzake waendelee mbele bila woga huku wakikumbuka misingi waliyowekewa wakiwa shuleni.

Mandhari

Mandhari ya shairi ni ya kuhitimu—yaani hali ya sherehe, tafakari na matarajio mapya. Kuna mseto wa hisia za furaha kwa kufikia mwisho wa safari ya shule na huzuni ya kuagana na wenzake. Pia kuna mandhari ya maadili na kiroho, ambapo mtunzi anasisitiza umuhimu wa kujiepusha na maovu na kuendelea kuwa na msimamo thabiti wa kimaisha na kiimani.

Wahusika

Mhusika mkuu ni mtunzi mwenyewe ambaye ni mwanafunzi anayehitimu. Anazungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake na pia anawalenga moja kwa moja. Wahusika wengine ni walimu, wazazi, shule yenyewe na hata jamii kwa ujumla. Kuna pia mazungumzo ya moja kwa moja kwa mwanafunzi mwenzake au wenzake waliokuwa karibu naye, jambo linaloonyesha ukaribu na uhusiano wa kijamii uliopo kati yao.

Hadhira Inayolengwa

Shairi linawalenga wanafunzi wenzake, walimu, wazazi na viongozi wa shule waliowashika mkono katika safari ya elimu. Pia linaweza kuwagusa wanafunzi wengine wanaokaribia kuhitimu, washairi chipukizi, na yeyote anayevutiwa na fasihi inayogusa maisha halisi ya wanafunzi na mabadiliko ya maisha yao.

Msimamo wa Mtunzi

Mtunzi ana msimamo wa kuheshimu elimu, walimu, na mchango wa watu waliomsaidia kufika alipo. Anaonyesha kuwa kuhitimu si mwisho wa safari bali ni mwanzo wa maisha mapya yanayohitaji maamuzi ya busara. Anasisitiza maadili mema, kujiamini, bidii na kumtegemea Mungu. Msimamo wake unaakisi ukomavu wa kijamii, kiakili na kiroho.

14 1

Maoni ya Wasomaji

Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.

Andika Maoni

Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.

Ingia kwa Google ili kutoa maoni kwa jina lako.

Endelea kwa Google