Kawaida Ya Wake Wenza
Ukara • Hulka • Wanawake

Kawaida Ya Wake Wenza

Tarehe: Januari 1, 2010 - Kimani wa Mbogo

Kawaida Ya Wake Wenza

Nimetafiti huluka, za wazee kwa vijana,
Sijakosa huzunika, bongo zikaudhiana,
Si haba huhamanika, yatendwayo nikiona,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Wataishi kwa hamaki, mara wakafurushana,
Sera hawazikumbuki, utakuta watwangana,
Hugombania miliki, katu kuafikiana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Hukutana kwa hasira, vita vyao kuumana,
Hujiletea madhara, punde wangachokozana,
Nguo hubaki tambara, wajapo wakapigana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Nyumba hakuna amani, kwa michi watachapana,
Wawili hawaungani, vema wakaelewana,
Mume wao hulaani, upatapo wapindana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Wake hawaoni haya, takuta waangushana,
Vema hawatatuliya, wawe waaminiana,
Husema tabia mbaya, sana wakitukanana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Hufoka kwa ukelele, mate wakitemeana,
Waende nyuma na mbele, mikono wameshikana,
Upesi huku na kule, daima wavurugana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Hawafanyi zao kazi, mafumbo hufumbiana,
Mara waitane wezi, wakianza kulumbana,
Wenyewe hawaigizi, ukutapo watwaana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Hawatendi la huruma, mangumi yakipambana,
Hawaijui heshima, mbio wakifukuzana,
Huanguka husimama, kishaye watanyongana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Halipo hawatatenda, si ajabu kuchomana,
Mchana kutwa hushinda, wake wakifarakana,
Vituko wanavipenda, hubaki wametengana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

Hawanalo la furaha, hubaki wasumbuana,
Wataitumia siha, nguvu wanapopimana,
Hawalioni la raha, wasaa wa kupambana,
Kawaida ya wake wenza, hawakomi kugombana!

© Kimani wa Mbogo

Shairi hili linaelezea hali halisi ya uhusiano kati ya wake wakiwa ndani ya ndoa ya mume mmoja, ambapo migogoro na ugumu wa kuelewana ni jambo la kawaida. Shairi linabainisha mitazamo tofauti kuhusu jinsi wake hawa wanavyoshughulikia tofauti zao, wengi wao wakihisi maumivu na huzuni kutokana na kutokuelewana kwao. Hisia za hasira, huzuni na kukatishwa tamaa zinajitokezacontinously, zikionyesha kuwa ugumu wa maisha ya pamoja unawafanya wawe na hali ya kudumu ya ugomvi na kutokuelewana. Katika ujumla, shairi hyakuwa funzo kwa wahusika kujifunza namna ya kutatua tofauti zao ili kuleta amani kwenye familia zao.

Lengo kuu

Dhamira kuu ya shairi ni kuonyesha changamoto na matatizo yanayojitokeza katika ndoa za wake wengi. Mtunzi anataka kuwakumbusha wasomaji kuhusu umuhimu wa maelewano na upendo miongoni mwa wake, na jinsi migogoro inavyoweza kuathiri si tu wake wenyewe bali pia familia nzima.

Mandhari

Mandhari ya shairi hili inahusiana na muktadha wa kijamii na kifamilia ambapo wake wanashiriki katika ndoa za mume mmoja, hali inayowalazimu kushirikiana. Ni katika mazingira haya ya kimila na kijamii ambapo tofauti kati ya wake zinaweza kuzalisha ugumu wa kimawasiliano na unavyoweza kusababisha ugumu ndani ya familia.

Wahusika

Wahusika wakuu katika shairi ni wake wenyewe, ambao kwa pamoja wanakabiliwa na changamoto za kutokuelewana. Ingawa mume anatajwa, anabaki kuwa na nafasi ya pili katika migogoro hii, huku wake wakionyesha wazi hisia zao za hasira na kukosekana kwa amani. Wahusika hawa wanatoa taswira ya akina mama wanaoshikilia hisia zao na kujikuta wakigombana na kuumizana.

Hadhira Inayolengwa

Hadhira inayolengwa ni jamii kwa ujumla, hususani wanawake na waume katika ndoa za mume mmoja. Ujumbe huu unawafikia wale wanaopitia hali kama hizo ili wajifunze namna bora ya kutatua matatizo yao. Pia, shairi linaweza kuwa funzo kwa vijana wanaojipanga kuingia kwenye ndoa, kuwasaidia kuelewa changamoto zinazoweza kujitokeza.

Msimamo wa Mtunzi

Mtunzi anaonekana kuwa na msimamo wa kukosoa tabia za wake hawa ambao hawaonyeshi umoja wala heshima miongoni mwao. Anaonyesha kuwa njia mbovu za kutatua migogoro, kama vile ugomvi na kutukanana, zinawaudhi na kuleta madhara katika jamii. Kila wakati, mtunzi anahimiza haja ya kuimarisha mawasiliano na amani ili kuleta furaha kwenye familia.

32 0

Maoni ya Wasomaji

Bado hakuna maoni yaliyoidhinishwa.

Andika Maoni

Shiriki mawazo yako kwa heshima. Baruapepe yako haitachapishwa wala kuonekana kwa wasomaji.