Laiti Ningejua

Ilianza ka’ mzaha, imegeuka karaha
Donda  latoka usaha, kaiba yangu furaha
Nilibugia tufaha, meiponza yangu raha
Laiti ningejua!

Nimebanwa  sipumui, nyangumi ameninasa
Mamangu  sikusikii, nimevutwa na usasa
Wazee siwatambui, nayapapia ya sasa
Laiti ningejua!

Nahisi ja takataka, penzi meingia doa
Ka’ kopo nilitumika, machozi mengi natoa
Muhibu ukawa  joka, vunda ahadi ya  maisha
Laiti ningejua!

Nahisi kusalitiwa, matungu yamenisonga
Najuta  kukataliwa, kisasi sitakipanga
Ipo siku tajaliwa, ya kale nitayafunga
Laiti ningejua!

© Nyangara Mayieka

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!