Najuta Kukupenda

Moyo umeudhulumu, hauna tena amani,
Umeujaza kwa sumu, umebaki taabani,
Uliyekuwa adhimu, umepoteza thamani,
Machozi hayaniishi, karaha menishushia.

Baada ya raha dhiki, umefanya niafiki,
Hujanitendea haki, kupenda sitadiriki,
Kweli hayatabiriki, ukipendwa hupendeki,
Japo niliyavulia, kuoga sijadhubutu.

Najuta kukuamini, na kukupenda kwa dhati,
NIlikutia moyoni, kwangu ulitaka hati,
Ulipofuzu sikwoni, umeshanipiga buti,
Nimebaki matatani, raha tena mimi sina.

Napata zako habari, nipitapo vijiani,
Japo yakwako ni swari, hauniishi huzuni,
Mama wewe ni hatari, ungezaliwa porini,
Kazi yako kudhulumu, wavunjavunja hujali.

© Ebeneza Jibrian

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!