Nchi Yetu Yazimia

Mtima naufungua, mengi kuwaeleza
nanena lote kwa pua, nisije kuimezea
viongozi lichagua, wapate kututetea
nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

kampeni zilitimia, debeni tukaingia
kura zetu tukawapa, uongozi wakaingia
umati wa kama papa, sote tulishangilia
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

Ahadi kumi na mbili, manifesto sikia
ufisadi kipaumbele, afya na elimu pia
barabara hata reli, zote kwa siku mia
nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

moja mwaka mmeishia, ahadi zimetokomea
unga ni shilingi mia, sukari shilingi mia
wakulima wanalia, waziri kuwakosea
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

Madeni wametutosa, wananchi watudhuru
wanavisa na mikasa, kuzila zetu ndururu
upinzani wameinasa, hawapigi tena nduru
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

Viongozi hawa feki, na pia ni wafisadi
wamejawa unafiki, waizi wa yurobondi
katu hawatishiki, serikali chezewa kadi
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

Raisi wetu hakika, ofisini kalegea
Kenya imetingika, baharini kunusia
Baba Raila amka, upate kututetea
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

Wino mie nalegeza, minne mwaka salia
maulana tatuongoza, na uhai kutujalia
hekima tutaponza, wasaliti kuwalipia
Nchi yetu yazimia, nani wetu mkombozi

© Br. Koffi Brian

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!