Dunia Niikalie

Tumboni kwa vizalia, vilio navyo nalia,
Njiani kutupilia, njia yenye nyingi nia,
Machozi yanatokea, ninatoka kupitia,
Tumboni kuchekelea, ndio mwendo kunuia.

Guu moja nalitoa, jicho moja nanyofoa,
Kono moja nakatia, guuni nachechemea,
Hemahema natokea, kupambana ya dunia,
Tumboni kuchekelea, ndio mwendo kunuia.

Tumboni toka nalia, tumboni nakojolea,
Jichoni wanionea, akilini natulia,
Mbio nyingi ‘kimbilia, vilio vyote nalia,
Tumboni kuchekelea, ndio mwendo kunuia.

Mama yangu jitolee, maisha yaelezee,
Kwa mengi uyatolee, amali uzipokee,
Kwa wajao wazilee, kwa kweli wasijutie,
Tumboni kwa hatarie, dunia niikalie.

Kwingi mengi ni utii, si pembe dunia hii,
Amani yenye hakii, nguzo ya mlio tii,
Tawi lake la manii, zuri jema hujutii,
Ndilo zao jema nii, swali zote zi kwanii?

Maisha kama kioo, kwayo kwake ndio soo,
Mwendo mrefu wa poo, mojamoja kokotoo,
Mwisho nakshi kioo, ishi kwa kujaza vyoo,
Ndilo zao jema nii, swali zote zi kwanii?

Waja wengi ni vibuu, ruko nyingi zao puu,
Hitima zao zi fyuu, hazina hata makuu,
Potozo lao li juu, shangazo zao keleu!
Ndilo zao jema nii, swali zote zi kwanii?

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!