Duniani Hangaika

Ukipigwa u pigika, ukisemwa u semeka,
Ukinena u neneka, ukiandikwa andika,
Umoja huja kutika, kuu zaja afrika,
Ukimya kunyamazika, maisha kuhangaika.

Polepole uchekeke, kimyakimya usomeke,
Kwa makeke ulimike, lawama nazo utwike,
Kwa uhondo upigike, pasi mwisho uneneke,
Maishani uchanike, mwingimwingi ushoneke.

Ratiba zako hakiki, zisiende kwa mkuki,
Angalizo lihakiki, neema kutoka tiki,
Mwendo usio na chuki, kila siku hutandiki,
Maishani huna dhiki, Mungu mmoja riziki.

Ishi maisha ya kiko, tumika vyema katiko,
Lakabu a lalamiko, andaa zilo tandiko,
Milenia we kumbuko, ajuza awe maziko,
Maisha dunia ziko, kusudi jema kitako.

Tumboni maisha chuku, duniani kuwa kuku,
Hangaiko la usiku, ama kweli hukuhuku,
Kumalizana kibuku, maisha gandamo teku,
Gonjwa kubwa la uziku, lenye tiba la maziku.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!