Dunio sio Kibaba

Haba na haba si haba, wazazi mama na baba,
Lalama na dhambi toba, haifai kwa kuziba,
Maisha siyo katiba, palotoboka kuziba,
Maisha yana haiba, kamwe huiwezi iba.

Nirushe na unibebe, kwa kila meza niikabe,
Maisha sio ubabe, bali moja la kichebe,
Palipo tobo uzibe, na uone vishitobe,
Maisha ndicho kitebe, sumbuko zote zikabe.

Njia moja kwake bibi, kupitia kwa usubi,
Lengo lake la kabibi, jema kweli lenye habi,
Tumboni huna janabi, kwa dunia kwenda jobi,
Maisha mwendo tabibi, dunia lindo la bibi.

Si kila tundu ni tobo, vingine tambale bibo,
Juuze zake vizibo, zenye tepete la bobo,
Tobo la jicho gobo, shimo lijengalo tobo,
Dunia yenye matobo, maisha yake kizibo.

Ntafurahi na babu, kwa utani uso tabu,
Maisha si majaribu, hata ndoa huto tibu,
Ulizo nyingi si jibu, maanani u katibu,
Dunia ndiye tabibu, aso hira za kujibu.

Abed Anthony
“shimbolyo”

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!