Tudumishe Maadili

Nawaomba karatasi, machache kuelezea,
Nitamwanzia kudusi, shukurani kumwambia,
Mola uwe radhi nasi, dhiki kutuepushia,
Nawausia vijana, maadili tuyachunge.

Nawaomba karatasi, machache kuelezea,
Nitamwanzia kudusi, shukurani kumwambia,
Mola uwe radhi nasi, dhiki kutuepushia,
Nawausia vijana, maadili tuyachunge.

Kileo kina utamu, kiingiapo vizuri,
Lakini pia ni sumu, tena sio takdiri,
Upatapo yake hamu, piga magoti kwa siri,
Nawausia vijana,maadili tuyachunge.

Sigara unapuliza, gari moshi afadhali,
Machozi unatutoza, wengine tena hatuli,
Mumegeuka mauza, kwa kuumiza miili,
Nawausia vijana, maadili tuyachunge.

Kuna nyingine tabia, zinazozua karaha,
Utalaleshi sikia, katu haibui raha,
Utaipata zinaa, ubakiye unahaha,
Nawausia vijana, maadili tuyachunge.

Libasi nazo chungeni, mzivaazo bayana,
Za ndani zibaki ndani, hatutaki kuziona,
Zipo nyingine jamani, maungo zinzazobana,
Nawausia vijana,maadili tuyachunge.

Shababi ishike dira, daima usipoteze,
Ufanye yenye tijara, na wakuu wasikize,
Sifate yenye hasara, usije ukateleze,
Nawausia vijana, maadili tuyachunge,

© Moses Chesire (Sumu ya waridi) Kitale mjini