Januari Nenda Salama

Januari enenda zako, nenda na viboko vyako,
Ulichoma kama jiko, ukaasi maandiko,
Chunguza adabu yako, mwezi usio mashiko!
Umeliza vya kutosha, enenda tukapumue!

Nimeimba wimbo wako, ni magumu mambo yako,
Wewe mwezi nenda zako,usinipe kisonoko,
Nani akupe upako, ugeuze mambo yako,
Umeliza vya kutosha, enenda tukapumue.

Januari wewe mnoma, wengi tulipata homa,
Na ukatesa vinoma, nazo pesa zikahama!
Wengine na yao homa, naona haitahama,
Umeliza vya kutosha, enenda tukapumue.

© Joel Mburia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!