Tusiibe Mitihani

Tuko hapa kuwajuza,swala hili mekithiri,
Na wala si kuwatuza,wizi huu ni hatari,
Watahiniwa sikiza,mtupate kwa fahari,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

Njia hino si halali,sisi sote twatambua,
Haienendi mahali,sisi sote tukataeni,
Tukiwepo na akili, sote tujiandaeni,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

Kwa hodari alipanga,kuwashika walo wezi,
Na sheria akatunga,ya kutupa mazoezi,
Alibaki kisimanga,wanafunzi mabazazi,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

Ina uchungu jamani,kwa kukosa matokeo,
Kwayo sababu haini,kuiba kwa mapokea,
Za mwizi arobaini,chunga sifikiwe leo,
Saitoti twalillia,alipinga swala hili.

Kwa bibilia takuta, amri moja ni kwa wezi,
Nayo korti hitosita,kuwashika wachochezi,
Na wakati takupata,utabaki ombolezi,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

Tufanye bidii yetu, juvunie jasho letu,
Sipokula jasho letu, tunataka viso kwetu?
Mitihani ya kikwetu,tuifanye bila kutu,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

Twamuomba na jalali,amlaze pema peponi,
Metuacha na kibali,cha kupita mitihani,
Njia yake ni halali,bongo zetu kubaini,
Saitoti twalilia alipinga swala hili.

Kiditama tumefika,ombi letu mesikika,
Hivi sasa sisimuka,kuwa mbele wakibika,
Kwa miaka na mikaka,vizi huno tohusoka,
Saitoti twalilia,alipinga swala hili.

© Brian Mutambo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!