Muda

Muda wetu tarajia,haupo tena mekwisha,
Muda wa hii dunia,ni adimu unatisha,
Muda  unao wadhania,kumbe ni kujichosha,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda kwao matajiri,ungalikuwa mwingi mno,
Muda  muda mwisho hungejiri,wangalala kwa unono,
Muda  kwao makafiri,wangarefusha na mikono,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda wake mtahiniwa,umekwisha ni mchahe,
Muda kwa muajiriwa,tapotea kama cheche,
Muda na mtarajiwa, tasubiri ukuwache,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda wetu duniani,umekwisha nakwambia,
Muda baya masikini,utabaki na kulia,
Muda unaothamini,sipoteze na tumia,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda ukiwa mzee,tatamani kuwa mchanga,
Muda wacha nelezee,kwa mtu kwenye mchanga
Muda wenda na kazi,kichelewa huna zao,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda ungekuwa ghali,hata kuliko chakula.
Muda si tungeujali,na usingizi kutolala,
Muda huno si ajali,unashinda kwa hela,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

Muda wangu tamatini,naondoka bila shaka,
Muda wako uthamini,watoweka kwa haraka,
Muda wetu duniani,tatoweka ja kiraka,
Muda  kweli ngali kopwa,wanohela wangalipa.

© Brian Mutambo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!