Umaskini

Donda ndungu lisotiba, ufukara kukithiri,
Kukandamiza ratiba, na misiba hutujiri,
Huwa kama ndio mwiba, usodunga matajiri,
Masikini akipata, tako hulia bwataa.

Na hali kiokota, husingiziwa kaiba,
Na  maradhi kimpata, huwa kwake ni msiba,
Kwa kuomba hujikita, apewe hata akiba,
simwamshe alalaye, ufukara tampata.

Ukata huwa mbaya, nayo njaa ikizidi
Waja kuzaa vibaya, na kuongeza idadi,
Hali  hii nakwambia, hubadili iikadi,
Masikini hohe hahe, hana mbele wala nnyuma.

Pengo hili hurefuka, masikini matajiri,
Na utumwa huibuka, utumwa ,kukicha alfajiri,
Watoto kubabaika, na vijana majangiri,
Chanzo cha ukahabaa, ni ufukara wenzangu.

Hukosesha na heshima, na nchi kutaabika,
Na  kuzuka kwa ugema, huwa chanzo cha tabaka,
Mwanafunzi wacha soma, maishani taabika
Maghulamu mbwa koko, hujidai kwa kubaka.

Nami jini kurundika, waja wengi kuhamiya,
Kazi mbovu hujitwikwa, ikiwemo kuvamiya,
Swala hili fahamika, huwa mbovu kitabiya,
Hali nawapa suluhu, ya kukwepa ufukara.

Kwanza kupanga uzazi, pili kupanda mimea,
Tatu nalo ni wazi, mtu kujitegemea
Tuacgane nao wizi, kwa kuacha kuzembea
Wazo langu mwalipata, kikomo mie natua.

© Brian Mutambo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!