Wa Dhamana Mzazi

Wapi mtu wa maana, kama si yeye mzazi,
Alinizaa mimi mwana, kanipa mema malezi,
Kunitunza sitakana, hiyo likuwa kazi,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Kanibeba miezi tisa, bila kuchoka mzazi,
Na yeye hakunitesa, kwa kuniavya mzazi,
Lichotaka sikukosa, wakinilea wazazi,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Duniani linileta, nikiwa ni salimini,
Mzazi bila kusita, ukanilinda ‘tatani,
Chanjo na nikazipata, kunilinda maradhini,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Mafunzo we ukanipa, nguo chafu kubadili,
Kikosea kanichapa, adabu kawa akili,
Adhabu we ukanipa , makosa kaona mbali,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Kanisa kanipeleka, kiroho niadilike,
Chochote nilichotaka,ukanip miye peke,
Kiniita kaitika, kutii nikakutii peke,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Karo nayo kailipa,nifunzwe somo muhimu,
Kutia bidii kaapa, mbele ya wangu walimu,
Mafunzo bora kanipa, liyo kupata adimo,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Ukanipa mawaidha, kuihusu hii dunia,
Kanionya chenye radha,nisije kadidimia,
Haswa mienendo kadha, enzi hii dijitalia,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Mabinti ukanionya, ovyoovyo kuwachekesha,
Kamwe sikuwakusanya,hizo enzi za maisha,
Hata  kanionya nyanya, kicheza nzo taisha,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

Mzazi yu wamaana, na sitamtekeleza,
Yeye mtu wa dhamana, hata kiwa ajuza,
Kunilea likazana, uzeeni tamtunza,
Yu wapi mwingine mwema, kama siyeye mzazi.

© Samwel mwangi Gathia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!