Maisha ya Dhiki

Twasikitika wakenya, maisha yamekauka,
Yabadilika kiunyoya, gharibi hadi shariki,
Taabu yatutawanya, mithili moto wa nyika
Wananchi wambambanya ,ngalau pata riziki.

Majanga jaa furifuri,kila kuchao ni kilio,
Mbolezi sasa mboleri, kwenye tanga na tangio,
Twazunguka kisayari, kipeleka lisalio ,
Wananchi wambambanya, ngalau pata riziki.

Gharama ya maisha, bei ya bidhaa dhahabu,
Yaongezeka siku nenda, silimia staajabu,
Jeki tupiga msaada, samaria staarabu,
Wananchi wambambanya, ngalau pata riziki.

Ajarari haijali,yakata kamba mtima,
Kusafiri hakustahili hilo langu azima,
Tujali Mola twasali, njiani onea huruma,
Wananchi wambambanya, ngalau pata riziki.

Madhila nayo yatuma, asili magari yetu,
Wengi wabaki vilema, bali vifo vya watu,
Masikitiko ya dama, kumwagika huku kwetu,
Wananchi wambambanya ngalau pata riziki.

Ajira nayo adima ,kama i wali wa daku,
Kuipata kwea mlima, hata kiwa shahitiku,
Vyeti beba kila juma kitafuta huko huku,
Wananchi wambambanya, ngalau pata riziki.

Kabla muda kuisha, na kuondoka jukuani,
Nasema haya maisha, si ambayo twtamani,
Kwa hayo nahitimisha, hadhira  buriani,
Wananchi wambambanya, ngalau pata riziki.

© SAMWEL MWANGI GATHIA

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!