Hatua ya Maendeleo 

Amini msiamini, natamani msadiki,
Taifa letu jamani, la uwezo mantiki,
Tokana jengo bungeni, hilo ni funzo bariki,
Tukiendelea hivi, ruwaza takuwa kweli.

“Mui huja kuwa mwema”, kinukuu kwa wahenga,
Magereza shajitoma, maendeleo shalenga,
Kazi mbali wazisoma, wafungwa pia ulenga,
Tukiendelea hivi, ruwaza takuwa kweli.

Uhandisi lotumika, bunge mpya kulijenga,
Thibitisho Afrika, kudorora tati nanga,
‘Limwengu muwe hakika, duni taboda kitinga,
Tukiendelea hivi, ruwaza takuwa kweli.

Zabuni zikitolewa,vijana jitokezeni,
Kandarasi mkipewa, mzifanye kwa plani,
Uaminifu takuwa, watu watatutamani,
Tukiendelea hivi,ruwaza takuwa kweli.

© Samwel Mwangi Gathia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!