Kilio cha Wanyonge 

Hao wanyonge walia,kwani hawana haki,
Wana haki wasikia,za kuwalinda mantiki,
Nani wakuwasikia,wanalia kila wiki,
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote.

Mayatima wako pweke,wazazi waliwaacha,
Jamii kawapiga teke,na hata ikawakacha,
Maisha si teketeke,wateseka siku kucha,
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote.

Nao watu walemavu,binadamu mewakataa,
Hawanao utulivu,wanaomba kwenye mitaa,
Hawana ukakamavu,pia jamaa mewakataa,
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote
Walia zezeru pia,sababu ya rangi yao,

Walimwengu wawachukia,na wakajitenga nao,
Kwa mitego wawatia,na viungo kuzinduo,
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote.
Wanyonge wanalia,wasamaria mwapi?

Msada waulizia,mmewapatia upi?
Wajaribu kila njia,wamesaidiwa vipi?
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote.

Jameeni serikali,na wanyonge wametengwa,
Haki ni kitendawili,ambacho wametegewa,
Wakati umewasili,wanyonge haki kupewa,
Kilioo cha wanyonge,kisikizwe nasi wote.

© SAMWEL MWANGI GATHIA

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!