Vaeni Vema

Vaa vazi ukijuwa, viungovyo la funika,
Vaa siache maziwa, machoni kutazamika,
Vaa staha kuibuwa, kila siku ukitoka,
Vaa mwana na kueza,hishima yako idumu!

Vaa na zuri fulana, kitovucho ifunike,
Vaa pendeze Rabana, ndio hasa penzi lake,
Vaa ziso bana sana, kiwa uwa mtu mke,
Vaa bibi na kueza,hishima yako idumu!

Vaa rinda upambike, likuchukue muhibu,
Vaa gotini lifike, kutembea siwe tabu,
Vaa vema tamanike, baibui na hijabu,
Vaa mwenzi na kueza, hishima yako idumu!

Vaa fiche malaika, sishitue mabanati,
Vaa sache ukatoka, huo wako mlingoti,
Vaa sije aibika, ukaleta hatihati,
Vaa bwana na kueza, hishima yako idumu!

© Simon Bin Itegi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!