Hekaya za Abunwasi

Umekuwa ja sungura, zabibu kuzikwangua
Mashavu yamekufura, ya kwangu meyatua
Mbona hujui majira, ya kutangaa na jua?
Kila mchimba kisima, huingiya mwenyewee

Waniona kama jura, limbukeni taniua
Ujanja ni yako dira, nafsi  kuiatua
Ninaona nitagura, menichosha takutua
Kila mchimba kisima, huingiya mwenyewee

Juzi umetia fora, kwa ucheshi ulozua
Wapumbavu  kawapora, za mwillini kawavua
Lukuki umewakera, waapa watakuua
Kila mchimba kisima, huingiya mwenyewee

Nimesimama imara, mkakamavu mekua
Taibua nyingi sera, kwa mungu taomba dua
Za Abunwasi si nira, hinoo nimeamua
Kila mchimba kisima huingia mwenyewee

© Nyangara Mayieka