Sumu

Sumu hino sumu, yakereza ini
Sumu chungu sumu, nimo taabani
Sumu liza sumu, binti nifanyeni?

Nimemeza sumu, mejaa kooni
Tungu aka! Sumu, yalia tumboni
Naitapika sumu, ndani mashakani

Tema mengi sumu, barafu kadhani
Mbegu zako sumu, bafe mesheheni
Mwenza ndiye sumu, singii foleni

Donda hili sumu, lauma kichwani
Ngejua ni sumu, lo! Singetamani!
Mtume! ni sumu, ni makuruhuni!

© Nyangara Mayieka

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!