Usafi

Usafi jambo muhimu, maanani tuliweke
Moyo tusitie sumu, fundo la inda siweke
Sithubutu kuhukumu, mola takupiga teke

Maji kiona saumu, viroboto wakuteke
Tainyonya yako damu,  maswihiba wakucheke
Nduli tajia kwa zamu, usalie na makeke

Kinywa chako sukutua, kama beberu sinuke
Mavazi safi valia, chawa watachana mbuga
Kama wapenda kunguni, siyakung’ute malazi!

Nyumba tuzinadhifishe, Mbu wasiwe wenyeji
Malari hatatuona, afya bora tajenga
Vyombo kiwa safi , kombamwiko tafukuza

Tunyweni maji masafi, matunda tuyaosheni
Mikono siisahau, ing’arishe ingaee
Kipindupindu kolera, tutazika kaburini

Nawaageni kwaheri, sina shaka kaelewa
Usafi mtadumishe, mazingira tapendeza
Usafi jambo muhimu, hino ninasisitiza

© Nyangara Mayieka

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!