Geuko la Gizani

Mwanga mulika kisogo, ubongo mwendo kisago,
Unga chomozo msago, ishi ugumu wa gogo,
Kalio kama la figo, chini yake huna pigo.

Gizani chogo geuko, mithili bata mwandiko,
Umbea huna mdako, hadi hima kokoriko,
Hemo za mihangaiko, usaliti huwa choko.

Geuko hili gizani, huibua uhaini,
Kesho mwanga kubaini, makusudi ya utani,
Gizani mwanga azini, kusudio la sirini.

Geuko lao gizani, anguko lao mwangani,
Fasili ya maishani, maisha mwendo wa kani,
Watu hawana ya nani, watafutapo fukweni.

Hangaiko la mizani, usawa kuubaini,
Akili za tabaini, kuyatoboa maini,
Maisha usawa kwani? ama hangaiko zuni.

Geuko hili kumbuko, sio kulemba mwandiko,
Kumeza malalamiko, geuko kunyesha mwiko,
Gizani kuntu geuko, hung’amua jumuiko.

© Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!