Picha Yazungumza

Picha yazungumza, jua linapochomoza,
Angazo la kuangaza, picha isiyo na toza,
Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.

Macho yao kuyakaza, akili kugugumiza,
Kesho wataiunguza, wengine kutoiuza,
Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.

Jana yake ilikoza, sababu leo kupoza,
Picha moja ya pwaguza, picha akili panguza,
Mchoraji umekaza, waichora kwa vioza.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!