Athari ya Andishi

Athari ya andishi, amani malalamishi,
Jambishi sio tapishi, moshi wake uhuishi,
Nyendo za tarakinishi, yaleyale maandishi.

Andishi li maanishi, haiba i hatarishi,
Andishi ni andalishi, maanishi makinishi,
Nyendo za tarakinishi, yaleyale maandishi.

Andishi ni lainishi, maisha hayajarishi,
Jaribio makinishi, maisha yenye ng’arishi,
Nyendo za tarakinishi, yaleyale maandishi.

Takataka niokote, zenye irabu tokote,
Karatasi potepote, tango zote mana zote,
Athari zi kotekote, maandishi ya popote.

Nyuma mbele pia kote, maana zake ni zote,
Nyundo zinagonga kote, maandishi kiokote,
Athari zi kotekote, maandishi ya popote.

Andishi lazoa zote, amani za viborote,
Andishi labeba zote, enzi za maisha yote,
Athari zi kotekote, maandishi ya popote.

Andishi mahakamani, kuntu kama la nyumbani,
Andishi kuu mbinguni, ni ng’atuko la dhambini,
Athari zi kotekote, maandishi ya popote.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!