Nami Sikuwa Sahihi

Nami sikuwa sahihi, maisha kuyafasihi,
Amko la asubuhi, lilifanya nyingi sihi,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Nayosema si mazuri, nyendo zake si shughuri,
Nazosema ni dhahiri, kauli zilizo shwari,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Jembe refu kwa uzuri, lina neema sanjari,
Panuo kwapo kaburi, ushujaa so kiburi,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Dudumizi domo zuri, meno yaliyofahari,
Ulimi wake wa shari, maneno jeusi pori,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Cheko sokoto vipori, huzuni unozo nzuri,
Damu chemko dhahiri, rangi zilizo shuhuri,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Jasho toko damu siri, puani ukeni pori,
Janga kubwa lenye pori, ng’amuo haba jasiri,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Chaniko nyingi fahari, jogoo beba fahari,
Nukio nyingi pozari, pilau ama uturi,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Ombi angalizo zuri, hemo la mwisho pondari,
Ombi ishio bahari, kifo didimo dodori,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Goti kupigwa vizuri, heshima kuifikiri,
Inamo sujudo ari, la hitima ilo shwari,
Miaka mingi husihi, maisha kwenda sahihi.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!