Dunia Mwendo wa Jala

Nahitaji sana kula, pumziko kwa kulala,
Baada ya zote sala, niamke kwa jalala,
Nipambanue kwalala, maisha kuyapatala,
Maishani tamu nala, dunia mwendo wa jala.

Niivishe na nikule, nawe uje na mchele,
Maisha siyo kelele, kuvifikia vilele,
Bali kuishi vichele, kung’amua ya milele,
Chakacho isha kelele, dunia ndelemo jele.

Haya hayana dalali, maisha kama jabali,
Kutoboa jikubali, tafakuri zote hali,
Tofauti za dalali, pambanuo ni akili,
kuishi kwangu kibali, maisha hatari duli.

Nyama zile holoholo, zi tengano kama cholo,
Nyingi huenda chololo, kwa mwendo usio kilo,
Zijiachapo kibilo, nafsia kwayo dolo,
Maisha mengi dololo, dunia haina mlo.

Ndondondo sio chululu, maisha mwendo wa telu,
Kuishi kwingi si lulu, teule ya jangwa belu,
Ing’aayo kama balu, amana yake katulu,
Maisha mwendo wa balu, dunia ni moja malu.

Abed Anthony
(Shimbolyo)

Maoni 1

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!