Mama Usimdharau

Libeba miezi tisa, tumboni pasi kuchoka
Mateso yote kabisa, mama haniachi kaka
Dada sikia wasia, sikia pasi kuchoka
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Kanipata kwa karaha, raha kabisa kakosa
Lake nipate furaha, nisihangaike hasa
Yake kawa ni buraha, isodumu kama kasa
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Mikosi alipitia, toka kuzaliwa kwangu
Mizigo alifikia, maisha yazidi kwangu
Kisha nilipokulia, kawa wa muhimu kwangu
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Maisha yalitubana, nyikuhi hadi nyingine
Tafuta alikazana, tupate hiki chengine
Mali alitafutana, ajaze tena mengine
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Mamangu alijikaza, vibarua katafuta
Toka shamba la baraza, hadi solo atafuta
Rohoni kajihimiza, nyiku moja
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Sikuli kanipeleka, masomo nikayapate
Nikafurahi fanaka, mtihani kaupite
Kwa miaka na mikaka, hadi nikavishwa pete
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Nilivyozoea mamangu, dada kaka wote kando
Yeye wa maana kwangu, dhahabu iweke kando
Maishani mwote kwangu, alipata langu pendo
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

Name nafunga shairi, machozi yananitoka
Nakosa vyake vizuri, nasema kwa uhakika
Nakuombea mazuri, pemani ulipofika
Mama usimdharau, heshimaye mpatie.

© Ouma wa Opata
(Malenga wa mjini)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!