Ni Wapi Tumekosea?

Wafisadi watuua, kemikali watwekea,
Sukari nimesikia, makuli wametwekea,
Sasa mchele murua, sumu wametutilia!
Mnataka kutuua, ni wapi tumekosea?

Mafuta sijasahau, yana sumu kweli pia,
Sukari siitumii, markuri yanitishia,
Mwataka wangu uhai, bure mwataka tuua,
Mnataka kutuua, ni wapi tumekosea?

Kumbukeni nyinyi pia, mtapoteza uhai,
Hivyo nyie hamfai, kujaribu kutuua,
Sana tutawaombea, sumu iwadhuru nyie,
Mnataka kutuua, ni wapi tumekosea?

Mengine siongezei, ninajihisi kulia,
Utu umewondokea, hamthamini uhai,
Nasi tutapiga dua, kuzimu mtangulie,
Mnataka kutuua, nanyi mtatangulia!

© Stephen Muia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!