Soma Kisasa

Soma mwanangu usome, elimu mwanga dhahabu,
Soma na utie shime, elimu ina adabu,
Penye elimu useme, kwa busara ya kibabu,
Elimu hino ni Pana, bahari lisilo mwisho.

Funzika kuzikatia, herufi usitarabu,
Ukitaka kwandikia,andikia taratibu,
Na unapowaimbia, waimbie taarabu,
Jielimishe shuleni, soma pia umatini,

Mwana wangu jichezee, kijipira chenye tyubu,
Kabumbu uwagongee, misuli yako kutibu,
Somo ulielewee, fikira zikose tabu,
Pa skuli Pana somo, Pa uwanja elimika.

Ufunzwacho ukipate, tolea nyingi sababu,
Ng’amua elimu yote, hata iwe ni hesabu,
Nakuasi pasi tete, maswali yote kujibu,
Ku mtihani wa shule, na mitihani ya maisha.

© Mwangi wa Githinji
(Malenga wa mchanga Kati)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!