Nachukia…

Mtimani nachukia, asosema waziwazi,
Arukarukae pia, mnazi hadi mnazi,
Wasiwasi anitia, kupenda napata kazi. 

Mtimani nachukia, mpenzi mwenye ghasia, 
Asiyetaka sikia, lolote nalomwambia, 
Asiyejali hisia, toka moyo kimwambia. 

Mtimani nachukia, mke mzabizabina, 
Anayependa umbea, na apendaye fitina, 
Siri kwa watu kutoa, ‘kanikalia kigwena. 

Mtimani nachukia, binadamu mwasherati, 
‘Sojua ni maasia, kufanya uasherati, 
Maradhi takuletea, na tikiti ya mauti. 

© Justine Bin Orenge

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!