Taaluma ya Ushairi

Kitabu kilicho chema, hakika nimekisoma,
Kila ninapokisoma, unatulia mtima,
Nacho ni cha taaluma, ya ushairi nasema,
Hongera Bwana Kitula, kwa hichi kitabu chema.

Kila ninapokisoma, chanifunza mambo mema,
Ushairi ulo mwema, chanifunza nikisoma,
Chanipa pia hekima, kukisoma sitakoma,
hongera bwana Amata, kwa hichi kitabu chema.

Wanafunzi mnasoma, someni vitabu vyema,
Hasa hii taaluma, yawafaa nyinyi vyema,
Nawaomba kufanya hima, kitabu hichi kusoma,
Hongera bwana Kitula, kwa hichi kitabu chema .

Mengine sitayasema, yametosha niliyosema,
Mashairi yalo mema, humo ndani utasoma,
Nawe ‘tajazwa hekima , useme ninayosema,
Hongera bwana Amata, kwa hichi kitabu chema.

© Stephen Muia Musau
(Malenga Mneni) Juja, Kenya

Maoni 1

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!