Ishara

Meingia mahabani, kwa mtu asiyejuwa,
Humuona kwa ndotoni, pendo amelichukua,
Kishituka kitandani, simuoni wa muruwa.

Laazizi laazizi, hali yangu waijua,
Meniacha kitandani, nina homa naugua,
Nilikosa karatasi, kukwandikia baruwa.

Hizi ni Aahabu gani, mimi zilizo nifika,
Nimekua matesoni, kutwa kucha nasumbuka,
Namuomba Kwa hisani, awe wangu kwa haraka.

Namshukuru Moliwa, kuwa yu pamoja nami,
Nae anganiringia, mwenzangu muambieni,
Kama mapenzi yauwa, kwanza ningekufa Mimi.

© Rajab Omar

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!