Biriani

Mwenza unuse hewani, yatamba harufu nzuri,
Sebule hata jikoni, sakafu na kwenye dari,
Kotekote na chumbani, pua yangu inakiri,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Uchanganyie masala,usisahau samli,
Utumie zako hela, chinje nyama ya fahali,
Uketi kwenye mswala, ule ‘Birani’ kamili
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Maisha ya siku hizi, ina mengi ya furaha,
Sherehe sawa na kazi, Kila siku kuna raha,
Chamcha naweka wazi, ipike bila kuhaha,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Mtoto akizaliwa,mgeni toka mbinguni,
Atakuja kulakiwa, awe furaha ya nyumbani,
Atapenda kupikiwa, maboga na biriani,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Vijana toka jandoni, kufunzwa Yale ya kunga,
Wonyeshe kuna uoendo, wakitoka kwa ngariba,
Welewe kuna uhondo, mchele wao kukonga,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Kwenye sherehe harusi, nikahi ya kata shoka,
Uwachinje mangisi, ama kanga wa kiyaka,
Fanya hima Fanya Kasi, Fanya wali kuchemka,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

Maisha ni hatua, kuna mwanzo kuna mwisho,
Mja akijifilia, ndio yake hitimisho,
Jipikeni Biriani, huo ndo wangu mpasho,
Biriani yapikika, mgeni wa shereheni.

© Mwangi wa Githinji
(Malenga wa mchanga Kati)

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!