Shukran Mama

Nafasi anga nipeni, nimsifu wangu mama,
Miezi tisa tumboni, kanibeba humo vyema,
Kavumilia tabuni, sababu kiwa huruma
Ninaona shani kubwa!

Tumesikia wahuni, wameua wao wana ,
Lakini mimi jamani, ninayo bahati sana,
Nakupongeza yamkini, takulipa Maulana
Ninaona shani kubwa!

Kanipeleka skulini, nipate ilimu bora,
Nifaidi maishani, nisije nikawa mkora,
Naye kwenye uzeeni, nimpe maisha bora,
Ninaona shani kubwa!

Nefikia tamatini, kushukuru wangu mama,
Wazazi heshimiweni, kwa kazizo zilo njema
Mwatukimu maishani, mbarikiwe kwa mema
Ninaona shani kubwa!

© Stephen Muia Musau

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!