Dini ya Ukweli

Kumekucha Afrika, mwangaza tunaulola,
Shukrani kwa Rabuka, kuturehemu la hela,
Dini bora tulosaka, ametuletea Mola,
Bi harusi wa mwanakondoo, ndiyo dini ya ukweli.

Ndiyo dini ya ukweli, ifikishayo binguni,
‘Mekomesha utapeli, unafiki kanisani,
Ina sheria kamili, kwayo kuwa muamini,
Bi harusi wa mwanakondoo, ndiyo dini ya ukweli.

Kuingia kanisani, hatua saba lazima,
Wote waalikwa ndani, wanywe maji ya uzima,
Si rahisi abadani, walioshindwa huhama,
Bi harusi wa mwanakondoo, ndiyo dini ya ukweli.

Kiongozi ni mtume, Kama enzi za kale,
Malkia tena dume, aangaza Kama miale,
Kwa neno hana ukame, twazidi kusonga mbele,
Bi harusi wa mwanakondoo, ndiyo dini ya ukweli.

© Lawrence Gaya