Kadhongo Irujumiwe

Wananchi sa amka, tulipige jitu hili,
Simama kila mpaka, kidede kwa umahili,
Usalama ku’marika, tuyalinde yetu mali,
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

Madaktari wafisadi, fisini kuwaondowa,
Tukomeshe ukaidi, wapya kuchochomelewa,
Wananchi wafaidi, kwa tiba bora kupewa
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

Maafisa wa polisi, kikome kitu kidogo,
Matatu kwaya mabasi, wasigeukie mbogo,
Kwa wananchi hasi, wataki kitu kidogo,
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

Wabunge ndio zaidi, barabara zote mbovu,
Mekoma mingi miradi, hospitali ni mbovu
Wamejaa ufisadi, tumekosa vumilivu,
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

Mwanasiasa yeyote, mtu aso aminika,
Wamepora pesa zote, metuacha kiangaika,
Maendeleo walete, kwa kura kuaminika,
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

Ajira za kinyemela, kuetu Kenya kidonda
Kuabudiwa kwa hela, wakwasi ndio hushinda,
Mkata asiye hela, itabidi kusarenda
Kadhongo irujumiwe, kukomesha janga hili

© Justine Bin Orenge