Pesa Pesa Ndio Wimbo

Naandika jambo hili, kwa heshima kubwa sana,
Hali yangu ni dhalili, Waleti yakia sana,
Nimejitia kwa seli, nisionekana sana,
Pesa pesa ndio wimbo, na njaa ni kibwagizo.

Benki nimeenda sana, ukutani kwangalia,
Roho inadunda sana, nadaiwa nakimbia,
Ngoja ngoja hii sana, Matumbo yaumizia,
Pesa pesa ndio wimbo, na njaa ni kibwagizo.

Tamaa ni kubwa sana, hata nyama nakwambia,
Nilikula mwaka jana, na mwaka sikuvukia,
Ngwenje ilikosekana, na Na sherehe sikungia,
Pesa pesa ndio wimbo, na njaa ni kibwagizo.

Kwangu tunaulizana, nini ilitukia,
Pesa pesa nzuri sana, lakini yanikimbia,
Mimi nangoja kuona, wikendi ishaingia,
Pesa pesa ndio wimbo, na njaa ni kibwagizo.

© Joel Mburia

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!