Ukata

Maswali najiuliza, wapi nilipokosea?
Kila siku najikaza, kazini nimepotea,
Buti nalo melikaza,, nasahau amkua,
Ukata nipige Vita!

Ukata umenikwida, nimeshindwa kupumua,
Ufakiri wa halida, nimeshindwa kuondoa,
Mejikaza kila muda, hela nipate pokea,
Ukata nipige Vita!

Kidogo nachokipata, kinikimu maishani,
Magenderi nayakata, kulima hata shambani,
Chochote takachopata, niridhike maishani,
Ukata nipige Vita!

Sitoikata tamaa, wala kuwa mwenye pupa,
Si kuwa mileonea, nalo’mba Mola kunipa,
La kutosha nalombea, asante mola kunipa,
Ukata nipige Vita!

© Justine Bin Orenge

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!