Usalama Wazorota

Usalama wazorota, vijana wamesumbuka,
Maendeleo kusita, hatari inapofika,
Popote huwezi pita, kwa hilo twalalamika,
Usalama kuzorota, ndicho chanzo cha uoga.

Serikali nauliza, kwa heshima na nidhamu,
Kilio changu napaza, usalama uwe humu,
Waziwazi natangaza, kilio changu muhimu,
Usalama kuzorota, ndicho chanzo cha uoga.

© Kimani wa Mbogo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!