Mnaona Mmefika

Mwanicheka mwanibeza, eti kuwa sijafika,
Uchi wangu mwatembeza, nafsi yangu kuiteka,
Ja kandanda mwanicheza, mwanirusha ka kiraka,
Siku yangu ikifika, wanadamu tanikoma.

Wanadamu tanikoma, wakomavyo ka la nina,
Tanienzi daima, sitokuwa vile tena,
Msamaha wa lazima, taniomba tena sana,
Siku yangu ikifika, tasifika kote kote.

Tasifika kote kote, ulayani na merika,
Jina langu kwayo yote, litakuwa lasikika,
Mie duni mniite, mimi kamwe sina shaka,
Siku yangu ikifika, nitacheka sitolia.

Nitacheka sitolia, ufukara sitotaja,
Tapenyeza ilo ndia, na kuvuka kwa daraja,
Tatimiza yangu nia, ya kuwa namba moja,
Siku yangu ikifika, na baraka miminia.

Na Baraka miminia, mola wangu nijalie,
Wewe kweli hudhuria, njia mbovu sipitie,
Wewe tena narudia, kwenye dhambi niondoe,
Siku yangu iafika,’kono heri tanijaza.

‘Kono heri tanijaza, hili ndilo langu ombi,
Tamatini najilaza, mambo haya ya wanangu,
Japo kuwa najiliza, mateso ya ulimwengu,
Siku yangu ikifika, ’ni kwaheri kuonana.

© Brian Mutambo

Maoni 1

 1. xxx

  Sіmpⅼy want to sаy your article is as amazing.
  The clarity in your ρut up is simply cooⅼ and i could think үou are knowledgeable ᧐n this subject.
  Fine with your permission allow me to ɡrab your feed to keеp սp to date
  witһ сoming near near post. Tһanks a million and
  please carry on the еnjoʏablе work.

  Jibu

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!