Pesa

Kila mtu atamani,pesa kwao ni maua,
Na kuzidi matamani,maua kweli huua,
Pesa kweli maishani,hata mwana anajua,
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Sarafu nio nasema, kutwa kucha hutakika,
Bila ngwenje tajiuma,hasaa msiba kijika,
Ndio karo ukisoma,na nauli kisafirika,
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Bila chapaa mi neleza,tungekuwa watu bure,
Maisha hatungeweza,singekula hata pure,
Pesa kweli sititiza,ndiyo nguzo pata shore,
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Pesa kweli natabiri,hiendani nalo penzi
Hivi sasa nahubiri,penzi bora ulienzi,
lisivunde  kwa  kadiri , kuvamiwa nao inzi ,
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Waweza kosa furaha , hata ukiwa tajiri,
Tabakia kwa kuhaha , kukicha alfajiri,
Na kupigwa na maisha,kila siku ikijiri,
Waweza kosa furaha , hata ukiwa tajiri.

Heri kuwa masikini,na uishi kwa amani,
Jipatie masikani,na kujipa  tumaini,
Kwa mabonde milimani,tapitia maishani,
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Pesa kweli ndicho chanzo cha maovu duniani,
Sanasana ndio mwanzo,wa ulafi matamani,
Sarafu ndio mwongozo,kila kitu maishani
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

Beti nane natulia,hata kama una hela,
Hivi sasa najulia,tutukuze wetu mola,
Kwani ndiye ajalia,tulapo na tukilala
Mwenye hela ni tajiri,asohela masikini.

© Brian Mutambo

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!