Mwenzio Mpende

Kamwe simghadhabishe, la kweli mwonyeshe penzi,
Muenzi na umvishe, simwaibishe mpenzi,
Ishi naye umlishe,silale njaa mpenzi.
Mpenzio raha yako, milele mwonyeshe penzi.

Siketi naye vibaya, ndio asije udhika,
Usimwonyeshe ubaya, asije kughadhabika,
Milele mpe hidaya, kwa raha tafarahika,
Mpenzio raha yako, milele mwonyeshe penzi.

Epuka uasherati, uwe mwaminifu kwake,
Umtengee wakati, wa kufurahia nake,
Tena usimsaliti, kamwe usimtoroke,
Mpenzio raha yako, milele mwonyeshe penzi.

© Samuel Nguru Mwangi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!