Raisi Wetu Uhuru

Mechi nne wazalendo, kwa uhimizo wa Mola,
Piga kura kwa upendo, na kumchagua ngula,
Uhuru Kenyatta pendo, kachukua utawala,
Rais Uhuru Kenyatta, shukrani nyingi kwako.

Daawa mjini Hegi, rais ukahimila,
Tunaungana kisigi, kutangaza zake lila,
Rais wetu si mbugi, jambazi kuwafadhila,
Rais Uhuru Kenyatta,shukrani nyingi kwako.

Wote walio hasimu, walio kwa utawala,
Kuwa mshonde ni sumu,tajutia masiala,
Uelewano muhimu, uadui ni ufala,
Rais Uhuru Kenyatta, shukrani nyingi kwako.

Matatizo meyakumba, migomo na masiala,
Tatua pasi kuyumba, maovu kaliliwala,
Sheria kwetu ni nyumba, taijenga kwa jamala,
Rais Uhuru Kenyatta, shukrani nyingi kwako.

Kwa historia ya Kenya, wa kipeke’ mtawala,
Ruto daima mkenya, kamwachia utawala,
Ghaidi mewatapanya, kwa ala toolatola,
Rais Uhuru Kenyatta, shukrani nyingi kwako.

Uhuru kuwa jadidi, Kenya tunajitawala,
Hegi kakosa ‘shahidi, kamwacha wetu ‘tawala,
Kota sheria shadidi, kamwe hana masiala,
Rais Uhuru Kenyatta, shukrani nyingi kwako.

© Samuel Nguru Mwangi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!