Joka Sugu

Joka hili linauma, kwa sumu inayoua,
Linaturejesha nyuma, ukweli nautasua,
Na midomo kayafuma, kaogopa kutoboa,
Wakenya tujihadhari, joka hili ufisadi.

Tukosapo kuhadhari, tamaka tumepotoka,
Tuiepuke hatari, hatari kufedheheka,
Iwe kati yetu ari, kulipinga hili joka,
Wakenya tujihadhari, joka hili ufisadi.

Joka linazorotesha, maendeleo ya nchi,
Tusikiri kuotesha, ufisadi wananchi,
Twahatarisha maisha, ‘jifisadi wananchi,
Wakenya tujihadhari,joka hili ufisadi.

Athari zinashamiri, kila uchao nchini,
Wako wapi washauri, watutoe taabani,
Simruhusu mshari, kututia kaburini,
Wakenya tujihadhari, joka hili ufisadi.

Mtoa kitu kidogo, na mkabidhiwa pia,
Tuwarudi si kidogo, na adhabu kali pia,
Yatengenezwe maago, takapopumzikia,
Wakenya tujihadhari, joka hili ufisadi.

© Samuel Nguru Mwangi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!