Penzi Lisilokomaa

Naandika kwa ghadhabu, vitendo vyako vyasinya,
Moyo mekosa tabibu, gonjwa lako menisinya,
Wanipa jina muhibu, nyonda wako kanifanya,
Nauepuka ubozi,mapenzi yasokomaa.

Nakosa umakinifu, darasani kila mara,
Sijielewi ja mfu, wazubaisha kisura.
Mahaba yafanye kifu, sikutaki kisura,
Yamenimaliza haya, mapenzi yasokomaa.

Waraka wazubaisha, meniteka nyara mie,
Nayaharibu maisha, tateseka bure mie,
Yaache yangu maisha, niyatengeneze mie,
Nahatarisha maisha, mapenzi yasokomaa.

Nayakataa mahaba, nachukua vitabu,
Naukataa uhaba, wa elimu ya vitabu,
Narudi kwa maktaba, za usoni siharibu,
Siku za usoni mbaya, mapenzi yasokomaa.

© Samuel Nguru Mwangi

Tafadhali usikose kuongeza Maoni yako kuhusu shairi hili.

Baruapepe yako haitaoneshwa hadharani. Maeneo yenye alama * ni lazima yajazwe!